Darasa La Ndoa

TZS 10,000.00
In stock
SKU
SpDarasa La Ndoa

Watu wengi hawajui maana halisi ya ndoa. Kukosekana kwa ufahamu huu ni chanzo kikuu cha mafarakano katika ndoa. Kwa msingi huu, ni muhimu kufahamu maana ya ndoa.

• Kisheria: Kufuatana na Sheria ya Ndoa ya Tanzania ya mwaka 1971, ndoa ni muungano wa hiari kati ya mwanaume na mwanamke, unaokusudia kudumu kwa maisha yao yote.

• Kikristo (Mw. 2: 24; Waefeso 5:31-33): Ndoa ni muungano wa pekee wa kudumu ambamo mume na mke wanakuwa mmoja tena. Ni kumkubali mtu (mume au mke) kuwa sehemu ya nafsi yako mwenyewe. Mke anakuwa sehemu ya mume na mume anakuwa sehemu ya mke, na hao wawili wanakuwa mwili mmoja.

“Alichokiunganisha Mungu, mwanadamuasikitenganishe” (Mk.10:9).

Ndoa ni wito wa kujitoa kwa maisha yote. Ndoa inamaanisha kuwa tangu wakati wa uchumba na Harusi na kuendelea, mtu anajitayarisha kushirikiana na mwenzi wake katika kila jambo;

Ndoa maana yake ushirika na ushirikishwaji. Ndoa ni ushirikiano, ambamo kila kitu ni mali ya wote na kinawahusu wote wawili katika ndoa. Vyote katika ndoa ni kwa ajili ya wote. Wanandoa wanashirikiana pamoja na kuchukuliana katika mapungufu na madhaifu yao.

Kushirikiana na kuwa na umoja katika hali zote za maisha; Mume na mke wanategemeana. Kila mtu ana mchango wake katika kufanikisha maisha ya ndoa; Ndoa ya Kikristo haiwezi kutenganishwa na Kristo aliye msingi wa ndoa. Yesu Kristo anahusika na ndoa zetu; Ndoa ya Kikristo ni ndoa ya Wakristo katika Kristo.

 

Links

Mungu ameanzisha ndoa kuwa taasisi ya msingi katika jamii, dini, na Taifa kwa ujumla. Hatuwezi kuwa na waumini na wanajamii bora kama ndoa hazitakuwa imara.

Hali ya ndoa nyingi si nzuri. Hakuna amani ya kutosha ndani ya familia nyingi. Idadi ya vijana wasioheshimu ndoa wala kuheshimiana katika ndoa inazidi kuongezeka.

Hali ya kuwajibika kwa wanandoa walio wengi ni kidogo sana na hivyo, kushusha thamani ya ndoa zenyewe.

Ndoto za wanandoa wengi wanapooana huwa ni kuishi pamoja hadi kifo kitakapo watenganisha. Vivyo, hivyo, wazazi wao, ndugu na jamaa hupenda kushuhudia wanandoa hao wakifanikiwa katika safari ya maisha yao ya pamoja. Hata hivyo, siyo wanandoa wote hutimiza ndoto hizo. Baadhi ya wanandoa wanaishi katika hali ya uchungu, mateso na visasi. Mafarakano na idadi ya ndoa zinazovunjika inazidi kuongezeka.

Utafiti unaonesha kuwa, kiwango cha talaka nchini Tanzania kimeongezeka kutoka asilimia 1.1 mwaka 2008/09 hadi asilimia 2.1 mwaka 2014/15. Baadhi ya ndoa zimedumu muda mfupi chini ya mwaka mmoja.

Hali hii haiathiri tu wanandoa husika, bali familia nzima ikiwamo zile zilizozalisha wanandoa. Aidha, hali hii ni hatari kwa mustakabali wa Taifa ikizingatiwa kuwa, ndoa ni moja ya taasisi muhimu za kujenga upendo, amani na mshikamano.

Kitabu hiki nimekiandika baada ya kutimiza miaka 25 ya ndoa yangu. Katika muda wote huo, nimejifunza mambo mengi na kupata uzoefu mkubwa.

More Information
Seller MLYUKA BOOK STORE
Author Rev.Dr. Enock Emmanuel Mlyuka
Total Pages 172
Publisher Pathfinder Image
Write Your Own Review
You're reviewing:Darasa La Ndoa
Your Rating
Copyright © 2023 - 2024 Mahali Sokoni Trading Company Limited. All rights reserved.