Imani ya Kuomba Mpaka Kupokea na Mwl. Eng. Peniel Sarakikya
Maudhui ya kitabu hiki ni kufufua ari yako ya kuomba, na
kukupa mwongozo wa kuomba kwa usahihi. Somo
hililimefunua siri ya kuishi kwa utoshelevu kwa njia ya
maombi. Utajifunza Maelekezo ya Yesu Kristo kuhusu
Maombi. Utazijua Sifa za Imani ya Kuomba hadi kupokea.
Utaelewa Kanuni za Kuomba kwa usahihi.
Utajua Vikwazo vya maombi yako na namna ya
kukabiliana navyo. Kupitia somo hili utajifunza Umuhimu
wa Kumpa Roho Mtakatifu nafasi katika maombi yako.
Utatambua majira na wakati ufaao kumwomba Mungu na
Umuhimu wa kujiwekea akiba ya maombi.
Kuna wakati ubongo hubishana na moyo juu ya uhalisia
wa tatizo fulani. Moyo hukaa na hisia na ubongo hukaa
kwenye ukweli.
Mabishano ya pande hizi mbili yakiwa makali, Mungu
huingilia kati kushawishi taratibu, lakini shetani
hulazimisha kwa nguvu matakwa yake.
Ubongo hufika mahali na kusema "litakalo kuwa na liwe",
moyo nao husema "tatizo bado halijaisha".
Katika mazingira haya, wale wanaokumbuka kuutafuta
uso wa Mungu kwa maombi huibuka washindi, na wale
wanaoishia kuwaza sana bila kuomba hukata tamaa
Hakuna mwanadamu aliyetosheka. Kila mmoja wetu ana
kitu cha ziada anachotafuta. Watu wengi hutumia juhudi
za kimwili kutafuta wanayohitaji, lakini wengi hukosa
kutokana na sababu nitakazokueleza katika kitabu hiki.
Wapo ambao hukosa kwa sababu hawamwombi Mungu
kabisa. Wapo ambao hukosa kwa sababu huomba
vibaya.
Maudhui ya kitabu hiki ni kufufua ari yako ya kuomba, na
kukupa mwongozo wa kuomba kwa usahihi. Somo
hililimefunua siri ya kuishi kwa utoshelevu kwa njia ya
maombi. Utajifunza Maelekezo ya Yesu Kristo kuhusu
Maombi. Utazijua Sifa za Imani ya Kuomba hadi kupokea.
Utaelewa Kanuni za Kuomba kwa usahihi.
Utajua Vikwazo vya maombi yako na namna ya
kukabiliana navyo. Kupitia somo hili utajifunza Umuhimu
wa Kumpa Roho Mtakatifu nafasi katika maombi yako.
Utatambua majira na wakati ufaao kumwomba Mungu na
Umuhimu wa kujiwekea akiba ya maombi.
Ni maombi yangu, kwamba Roho Mtakatifu
atakuwezesha kuelewa na kuutendea kazi ujumbe huu.
Mwl. Eng. Peniel S. Sarakikya
April 2024
Seller | SARAKIKYABOOKSTORE |
---|---|
Author | Mwl. Eng. Peniel Sarakikya |
Total Pages | 141 |
Publisher | Kiwonyi Printers |
-
Knowing Jesus Christ by Mwl. Eng. Peniel SarakikyaTZS 10,000.00