Kufikia Imani by Mbiso
Mchungaji Mbiso anaeleza sawa kwamba kuna imani ya kiMungu na imani ya kibinadamu. Maelezo ya mwandishi huyu kuhusu aina hizo mbili za imani yanatoa mafundisho mazuri sana kwa mkristo, soma uone. Pia, anaeleza kuwa kuna imani kubwa na ndogo, imani imara na dhaifu. Katika hali nyingine imani inaweza kuwa hai au iliyokufa.
Mwandishi huyu anasema kwamba mtu aweza kuwa na imani ndogo katika eneo moja na akawa na imani kubwa katika eneo jingine. Soma kitabu hiki utaona na kujipima; Kitabu hiki Namna ya Kuamini kwa Kutarajia Yasiyoweza Kutarajiwa.
Mwandishi huyu anasema kwamba imani ni kipawa toka kwa Mungu, kwamba imani ni mkono wa kupokelea toka kwa Mungu kile Mungu alichonacho kwa ajili yetu. Hata hivyo, mwandishi anakubali kwamba imani inapambana na changamoto mbili kubwa. Moja ya changamoto hizo ni elimu ya sayansi au hali halisi inayoweza kueleza tofauti na mtu anavyoamini. Sayansi inataka jambo liwe na uthibitisho, tofauti na imani. Changamoto nyingine ni majaribu. Natoa wito kwa msomaji wa kitabu hiki akisome kwa makini kitampa ufahamu wa mambo hayo muhimu katika imani.
Seller | MBISOBOOKSSTORE |
---|---|
Author | Rev Allen Adam Mbiso |
Total Pages | 80 |
Publisher | Rev Allen Adam Mbiso |