Mambo 15 ya Kujadiliwa kwa Wanandoa Watarajiwa Na Mchg Isaac Challo
Uchaguzi wa mwenzi wako wa maisha utaathiri vitu vingi katika maisha yako. Aina ya maisha utakayoishi, aina ya watoto na familia utakayoanzisha inategemeana sana na aina ya mwenzi utakayemchagua kuanza naye maisha.
Uchaguzi wa mwenzi wako wa maisha utaathiri vitu vingi katika maisha yako. Aina ya maisha utakayoishi, aina ya watoto na familia utakayoanzisha inategemeana sana na aina ya mwenzi utakayemchagua kuanza naye maisha. Kwa kuwa maamuzi haya yanagusa maeneo yote ya maisha yenu, ni busara sana kuweka msingi na dira au ramani itakayobeba ndoa inayotarajiwa kuanza hapo baadae. Mjadala huu ni sawa na kuunda katiba au muongozo utakao epusha migongano ambayo inaweza kudhoofisha ndoa yenu. Ndoa bora haitokei tu pasipo jitihada za kukusudia na maandalizi ya maana. Ndoa ni mwanzo wa safari yenye matukio mengi. Ndoa zina mishangazo mibaya na mishangazo mizuri. Kujua toka mwanzo na hasa kabla hamjaanza kuishi pamoja baadhi ya vitu mtakavyokutana navyo na vitu mnavyoweza kukutana navyo vitawaponya na maumivu yatokanayo na migogoro katika ndoa. Kwa kuwa ndoa yeyote iliyobora ina kanuni na misingi bora, kitabu hiki kimekusudia kukupa misingi ya kuifanya ndoa yenu inayotarajiwa iwe na matokeo na mguso chanya kwenu na kwa uzao wenu na jamii mtakazokuwa na maingiliano nazo. Karibu tujifunze pamoja.
Seller | ISAACBOOKSHOP |
---|---|
Author | Pastora Betty Challo. |
Total Pages | 32 |
Publisher | Truth Printing. |