Mavazi Yanavyo mtambulisha mtu By Mwl Caleb Mathias
Vazi ni kitu kinachovaliwa mwilini kama vile nguo au ngozi. Lengo kuu la kuanzishwa kwa vazi hususani nguo au ngozi ilikuwa ni kusitiri mwili ili uchi wa mtu usionekane katika macho ya kila mtu.
Kwanini tunavaa nguo? Tunavaa nguo ili kusitiri miili yetu, lakini pia tunavaa nguo sababu ya wengine. Ndio maana ukiwa chumbani kwako unaweza ukabaki uchi na hakuna anayekusumbua, lakini huwezi ukatoka hivyo hivyo ukaenda mjini, utaonekana umechanganyikiwa.
Kwa mara ya kwanza kabisa vazi lilitambulishwa na Mungu mwenyewe baada ya Adamu na Hawa kumtenda Mungu dhambi na kufumbuliwa macho yao na wao kuanza kujiona wako uchi.
Mungu alimchinja mnyama kisha akatwaa ngozi ya mnyama huyo akawatengenezea vazi ili kusitiri miili yao. Hii maana yake ni nini?
Maana yake ni kwamba, uchi wa mtu yeyote kwa namna yeyote haupaswi kuonekana machoni pa watu wengine isipokuwa kwa mke na mume.
Mungu aliendelea kuachilia maarifa kwa Mwanadamu aliyemuumba juu ya utengenezaji wa mavazi ya kusitiri.
Seller | CALEBBOOKSTORE |
---|---|
Author | Caleb Mathias |
Good Read | Yes |
Total Pages | 52 |
Publisher | Askofu Fredick Simon |