Mazungumzo Kabla ya Ndoa
Ndoa ya Kikristo ni ndoa inayotegemewa kuwa ya kudumu na isiyokatishwa na talaka. Kwa mujibu wa maandiko ni kifo tu ndicho kinatangua agano na unganisho la ndoa .Ndoa ni mwanzo wa safari yenye matukio mengi.
Ndoa ya Kikristo ni ndoa inayotegemewa kuwa ya kudumu na isiyokatishwa na talaka. Kwa mujibu wa maandiko ni kifo tu ndicho kinatangua agano na unganisho la ndoa .Ndoa ni mwanzo wa safari yenye matukio mengi. Ndoa zina mishangazo mibaya (bad surprises) na mishangazo mizuri (good surprises). Kujua tokea mwanzo vitu unavyoweza kukutana navyo baada ya kuoa na kuolewa vitakuponya na maumivu ya kushangazwa na vitu ambavyo hukutegemea vinaweza kutokea. Uzoefu unaonesha kuwa wanandoa wengi miezi kadhaaa na hata miaka kadhaa inayofuata katika maisha ya ndoa huendelea kugundua tabia na mazoea kwa wenzi wao ambazo hawakutegemea kwamba wangekutana nayo.Nyakati za mwanzo za urafiki, uchumba na wakati wa fungate (honey moon) mara nyingi wanandoa huishi maisha bandia pasipo kudhihirisha tabia na mienendo halisi ya jinsi walivyo. Siku zinavyoongezeka ndivyo mtu halisi huanza kujitokeza. Baada ya hapo kauli au mawazo ya sikujua kama mtu huyu yuko hivi. Fikra za kwamba laiti ningejua nisingejiingiza katika mpango huu. Na mara huanza kupata mwanya wa kudhani kwamba uchaguzi haukua sahihi. Uchaguzi wa mwenzi wako wa maisha utaathiri vitu vingi katika maisha yako.
Seller | ISAACBOOKSHOP |
---|---|
Author | Rev.Isaac E. Challo |
Total Pages | 84 |
Publisher | Moccony Printing Press |