Mchungaji na Uongozi by Rev Enock E Mlyuka
Mchungaji na Uongozi by Rev Enock E Mlyuka
Uongozi ni dhamana.Bila shaka wengi wetu tunafahamu kuwa kiongozi ni mwonesha njia. Lakini kiongozi bora haishii kuonesha njia tu, bali naye
hupita katika njia anayowaelekeza watu kuipita. Maana yake ni kwamba, lazima kiongozi awe mfano mzuri (role model) kwa wale anaowaongoza. Kiongozi bora anajua fika kuwa yupo kwa ajili na kwa niaba ya watu. Kiongozi anayejua hivyo, anajitambua kuwa yeye ni mtumish(servantleader) kwa anaowaongoza ili kufikia malengo yanayotarajiwa. John C.Maxwell, anaongeza akisema, uongozi ni ushawishi (leadership is influence). Ni uwezo wa mtu mmoja kuwashawishi wengine ili wamfuate. Anakumbusha kuwa, kila wakati kiongozi akiongoza, ageuke nyuma na kuangalia kama kuna mtu yeyote anayemfuata. Hata hivyo, ikumbukwe kwamba kuna wakati kiongozi ambaye ni mtu wa mabadiliko (dynamic), atalazimika kutembea peke yake kwa muda hadi watu waelewe anataka kufanya nini.
Seller | MLYUKA BOOK STORE |
---|---|
Author | Rev Enock E Mlyuka |
Total Pages | 124 |
Publisher | The pathfinder image |