Nami Nitakupa Wewe Funguo Za Ufalme Wa Mbinguni by Rev Allen Adam Mbiso
NAMI NITAKUPA WEWE FUNGUO ZA UFALME WA MBINGUNI
Lengo la kitabu hiki ni kukupa ufunuo wa mamlaka uliyonayo katika ufalme wa Mungu na namna ya kufunga yanayokutesa au usiyoyataka katika maisha yako na kufungulia unayoyataka na yatakayo kupa furaha ya kweli. Kwa maneno rahisi kitakusaidia kupata ufunuo wa namna ya kufanya ili kila yaliyo halali Mbinguni yawe halali katika maisha yako na yasiyo halali Mbinguni yasiye halali katika maisha yako.
NAMI NITAKUPA WEWE FUNGUO ZA UFALME WA MBINGUNI
Mathayo 16:19 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.
Haya ni maneno ya Bwana wetu Yesu Kristo akimuahidi Mtume Petro kuwa atampa funguo za ufalme wa Mbinguni na lolote atakalolifunga duniani likatukwa limefungwa Mbinguni. Vivyo hivyo lolote atakalolifungua duniani litakuwa limefunguliwa Mbinguni. Kifungu hiki kinaonesha kuwa kuna funguo zaidi ya moja ambazo Bwana wetu Yesu Kristo aliahidi kumpa Mtume Petro na Kanisa kwa ujumla wake. Ahadi hii haikuwa kwa mtume Petro peke yake bali ni kwa jamii ya waaminio yaani Kanisa la Kristo kufuatana na Mathayo 18:18 – 19. Biblia inasema; Amin, nawaambieni, yoyote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni. Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni (Mathayo 18:18-19).
Seller | MBISOBOOKSSTORE |
---|---|
Author | Rev Allen Adam Mbiso |
Total Pages | 101 |
Publisher | Rev Allen Adam Mbiso |