Nguvu Ya Maagano Saba Ya Mungu by Rev Allen Mbisso
Mungu Baba wa Mbinguni ni Mungu wa maagano, hufanya maagano, hufunua maagano, hushika maagano na hutuwezesha kushika maagano. Maagano ya Mungu katika Biblia hufunua upendo, rehema na fadhili katika shauri la Bwana juu ya mwanadamu. Ujasiri katika maombi ni kwa kuwa Mungu tunayemwabudu ni mwaminifu katika maagano aliyoyafanya. Nabii Daniel alipata ujasiri wa kumwomba Mungu asamehe uovu wa Israeli na kuwarehemu kwa kuwa alijua kuwa Bwana ni Mungu ashikaye maagano.
Wengi wamesikia juu maagano ya kichawi, maagano ya miungu na namna ya kushughulika nayo ili kupata ukombozi ila sio wengi waliopata nafasi ya kusikia kwa kina juu ya maagano aliyoyafanya Mungu na wanadamu katika Biblia. Silaha za ushindi zinazotumika kupambanana na maagano ya miungu zinatoka katika maagano ya Mungu muumba Mbingu na nchi, hivyo kujifunza habari za maagano ya Mungu na wanadamu kama yaliyoelezwa katika Biblia ni ushindi mkubwa dhidi ya maagano ya giza. Maagano aliyoyafanya Mungu yana nguvu kuliko maagano ya kishetani.
Seller | MBISOBOOKSSTORE |
---|---|
Author | Mch: Allen Adam Mbiso |
Total Pages | 90 |
Publisher | Rev Allen Adam Mbiso |