Nguvu ya Msalaba by Rev Allen Adam Mbiso
NGUVU YA MSALABA NA UFUFUKO WA YESU KRISTO INAVYOTENDA KAZI
Ninakushukuru wewe msomaji kwa kuamua kusoma kitabu hiki na kupokea kile ambacho Bwana Yesu Kristo amekuandalia ndani ya kitabu hiki. Tuungane na Mfalme Daudi anaposema katika;
Zaburi 145:1, Ee Mungu wangu, Mfalme, nitakutukuza, Nitalihimidi jina lako milele na milele.
NGUVU YA MSALABA NA UFUFUKO WA YESU KRISTO INAVYOTENDA KAZI UTANGULIZI
Ndugu msomaji, ujumbe wa kitabu hiki unalenga kutoa ufunuo wa kutembea katika nguvu za Mungu au kuishi maisha ya ushindi ndani ya ufalme wa Mungu. Msalaba wa Yesu Kristo ni msingi wa imani ya Kikristo, Wakristo wengi hawana ufunuo wa msalaba na kufufuka kwa Yesu Kristo kunavyotenda kazi katika maisha ya sasa, kwao msalaba ni jambo la historia na la siku ya mwisho. Hofu juu ya uchawi na nguvu za giza kwa Wakristo wengi ni matokeo ya kutokuwa na ufunuo juu ya msalaba au kupuuza msalaba wa Yesu Kristo.
Kwanza kabisa, kitabu hiki kinatusaidia kuangalia namna Bwana wetu Yesu Kristo alivyofanya huduma hapa duniani. Huduma ya Bwana Yesu Kristo ilikuwa na mambo makubwa yafuatayo; alifundisha na kuhubiri habari za ufalme wa Mungu, kusamehe dhambi, kuponya watukutoa pepo na kutenda miujiza. Huduma ya Bwana wetu Yesu Kristo haikuwa huduma ya maneno tu, iliambatana na udhihirisho wa yale aliyokuwa akifundisha na kuhubiri kama tunavyo soma katika;Matendo ya Mitume 1:1 Kitabu kile cha kwanza nalikiandika, Theofilo, katika habari ya mambo yote aliyoanza Yesu kufanya na kufundisha.
Seller | MBISOBOOKSSTORE |
---|---|
Author | Rev Allen Adam Mbiso |
Total Pages | 138 |
Publisher | Rev Allen Adam Mbiso |