Shetani Alitoka wapi
Jina la Shetani ni jina linalofahamika sana kwa watu wenye dini na wasio na dini.Ni jina linalohusishwa na uovu na uharibifu hasa katika nyanja za kiimani lakini pia hata katika matukio ya kawaida ya kila siku.
Jina la Shetani ni jina linalofahamika sana kwa watu wenye dini na wasio na dini.Ni jina linalohusishwa na uovu na uharibifu hasa katika nyanja za kiimani lakini pia hata katika matukio ya kawaida ya kila siku. Imani kuhusu uwepo wa Shetani na utendaji kazi wake ni kongwe na imerithishwa vizazi hadi vizazi tangu enzi za Adamu na Eva. Vitabu vya imani vya dini karibia zote duniani vimeweza kuelezea kwa sehemu fulani ubaya wa Shetani na kazi zake kwa wanadamu. Pamoja na jitihada za kuelezea kazi na ubaya wa Shetani, ni vitabu vichache vimejikita kuelezea kwa kina chanzo cha shetani na hatima yake.Kusudio la kitabu hiki ni kuelezea asili, anguko, kazi zake na mwisho wa Shetani katika tafsiri ya Biblia kama ilivyoainishwa katika Agano la Kale na Jipya. Kusudio la pili ni kuelezea ushindi mkuu kwa wana wa Mungu (Yohana 1:12) dhidi ya Shetani kupitia kifo cha Yesu pale Msalabani na kufufuka kwake.
Kwa msaada wa vyanzo mbalimbali na kwa mitazamo ya wanazuoni wengi wa Kikristo duniani, nakualika kwenye ufafanuzi wa Neno la Mungu juu ya Shetani, asili yake, anguko lake, kazi zake na mwisho wake. Kupitia ufafanuzi huu utaongeza ufahamu wa Neno la Mungu utakao kusaidia kumjua Mungu na mpango wake mtambuka wa kumrejesha Mwanadamu katika mahusiano hasa baada ya Shetani kujaribu kuvuruga mahusiano ya Mungu na mwanadamu. Ufahamu huu wa Neno la Mungu utakusaidia kumjua Mungu na kumpenda Yeye aliyetuumba na kutuandalia ushindi usio na shaka dhidi ya Shetani kupitia Yesu Kristo.
Seller | ISAACBOOKSHOP |
---|---|
Author | Rev.Isaac E. Challo |
Total Pages | 102 |
Publisher | Moccony Printing Press |