Shughulikia Hofu Na Caleb Mathias
Shughulikia hofu hizi ili utimize ndoto zako
Maisha yako yanabadilika au kutokubadilika kwa sababu moja tu ambayo ni ujasiri, na ujasiri huo ni ujasiri wa kuanza kuchukua hatua, ujasiri wa kuvumilia mara baada ya kuchukua hatua na ujasiri wa kumaliza vitu ulivyovianza kuvichukulia hatua. Dawa ya hofu ya kitu chochote kile ni kuwa na ujasiri wa kuanza, ukiwa na ujasiri wa kuanza hofu itaondoka yenyewe, weka gia ya kuanza kwa ujasiri na hofu itakimbia yenyewe. Fanyia kazi mambo unayoyaogopa au mambo ambayo hauna ujasiri nayo. Ndoto zetu zinaweza kutimia ikiwa tuna ujasiri wa kuzifuata, ujasiri pekee mtu yeyote anaouhitaji ni ujasiri wa kuzifuata ndoto zake mwenyewe. Unaweza kuwa na ndoto ya kuwa mtu fulani lakini kama huna ujasiri wa kufanyia kazi utabakia kama ulivyo. Tunashindwa kuishi maisha tunayoyataka kwa sababu ya hofu, kitu kinachoua ndoto za watu wengi ni hofu. Wengi wetu hatuishi ndoto zetu kwa sababu tunaishi hofu zetu. Hofu ndiyo kikwazo kikubwa cha wewe kushindwa kufikia mafanikio makubwa. Kama
usipokuwa jasiri utapoteza vitu vingi ambavyo ni haki yako kabisa.
kitu.
Seller | CALEBBOOKSTORE |
---|---|
Author | Mwl: Caleb |
Total Pages | 124 |
Publisher | Kiza |