Tafsiri za kauli tata za Bwana Yesu By Pator Challo
Tafsiri za kauli tata za Bwana Yesu.
Maisha ya Yesu Kristo, tangu kuzaliwa kwake huduma yake, kufa na kufufuka kwake yamejaa matukio mengi ambayo yameleta mijadala mingi na mirefu vizazi hadi vizazi.
Ukifanya utafiti wa umaarufu wa watu katika nyanja mbalimbali kama dini, siasa, sayansi, falsafa na kadhalika huwezi kupata mtu mwenye historia ya pekee, ipendezayo na ya ajabu kama ya Yesu Kristo.
Dunia hii tangu kuumbwa kwake imeshuhudia watu wengi mashuhuri waliofanya vitu vikubwa (vizuri na vibaya), wakizaliwa, wakaishi na kupita.Historia ya watu hawa mashuhuri husahauliwa na pengine kutoweka kabisa baada ya wao kupita.
Umashuhuri na udhahiri wa Yesu Kristo katika huduma yake, uweza na nguvu zake ni hai leo kama zilivyokuwa nyakati zile.
Uwepo wa Yesu na kazi zake hapa duniani umebadilisha maisha ya watu, kiroho na kimwili tangu nyakati alizokuwepo duniani na anaendelea kubadilisha maisha ya watu hadi leo.
Seller | ISAACBOOKSHOP |
---|---|
Author | pastor Isaac Challo |
Total Pages | 84 |
Publisher | A & G 2005 Communications Limited |