Tiba ya ndoa
Mambo yanayosababisha msongo wa mawazo ni pamoja na pale mtu anapofanya mambo yasiyolingana na hali na uwezo wake alionao. Mfano, kujilinganisha na wengine. Hii ni sawa na mtu kuthubutu kujikuna mbali zaidi ya kimo cha mkono wake. Matokeo yake mtu anapata hofu na kupoteza matumaini ya maisha.
Tunaishi katika ulimwengu wenye Baraka na changamoto nyingi. Changamoto mbalimbali za maisha, Kwa sehemu kubwa, Ni kisababishi cha msongo wa mawazo. Kuwa na msongo wa mawazo ni hali ya kawaida na isiyoepukika katika maisha ya binadamu ya kila siku. Pamoja na madhara makubwa ya msongo wa mawazo, hata hivyo, msongo wa mawazo unaweza kutusaidia kubadili mitazamo yetu, mienendo na namna yetu ya kufanya mambo.
Msongo wa Mawazo ni nini? Ni hali ya kusongwa na mawazo inayotokana na hali za maisha ya kila siku. Msongo wa mawazo unaathiri mwenendo ( behaviour) na hisia ( feelings) za mtu nyumbani kwake, kazini na katika jamii kwa ujumla.
Athari zinaweza kuwa za muda mfupi ama za muda mrefu kutegemeana na kiwango cha msongo wa mawazo ( levels of stress) na pale msongo wa mawazo unapodumu kwa muda mrefu. Kwa hiyo, mada hii ni muhimu sana kwani inagusa maisha yetu ya kila siku. Katika mada hii, tutajifunza mambo matatu:
i. Visababishi vya msongo wa mawazo ( stressors); ii. Matokeo ya msongo wa mawazo ( consequences); iii. Namna ya kukabiliana na tatizo la msongo wa mawazo ( coping with stress).
Seller | MLYUKA BOOK STORE |
---|---|
Author | Rev,Dr. Enock E. Mlyuka |
Total Pages | 125 |
Publisher | Pathfinder Image |