Ufumbuzi wa Fumbo la Kiberiti
Ufumbuzi wa Fumbo la Kiberiti: Safari Ndefu yenye Ushuhuda
Katika kitabu hiki, Mhandisi James Mitayakingi Erasto Kilaba ametuonyesha namna ambavyo shauku,
azma, bidii kazini na kuishi kwa malengo vilivyomzawadia mvulana kutoka mojawapo ya vijijiji vya mkoa
wa Mwanza kuwa mtatuaji wa matatizo, kiongozi na mmoja wa waliochangia katika kuendeleza sekta ya
mawasiliano Tanzania.
Tunaona jinsi stadi zake na utashi wa kushiriki katika vikundi wakati akilima kwa kutumia jembe la
mkononi kwenye shamba la familia kijijini na pia katika vikundi vya kujisomea na wanafunzi wenzake
alipokuwa Shule ya Sekondari ya Ufundi Ifunda na Chuo cha Ufundi Dar Es Salaam ambacho sasa ni
Taasisi ya Teknolojia Dar Es Salaam.
Misingi hii iliimarishwa aliposhiriki shughuli za Shirika la Mawasiliano Ulimwenguni (ITU), chombo cha
Umoja wa Mataifa kuhusu TEHAMA, ambako alikuwa mjumbe na kiongozi wa kamati mbalimbali na pia
katika kushirikiana na wanavijiji wa Kitomonndo, mkoa wa Pwani ambako ana shamba.
Kupitia uzoefu wake na azma kubwa ya kushawishi na kutia moyo wengine kuhusu namna ya kutatua
matatizo kwa njia mbalimbali bila kujali changamoto zilizokuwepo; zikiwa zinatokana na mazingira ya
asili, mfumo wa ikolojia, Teknolojia ngumu kueleweka, masuala ya kiroho au hali halisi.
Mhandisi Kilaba amekitendea haki kitabu chake kwa kutusimulia namna alivyoifikia ndoto yake
kufumbua fumbo la kiberiti. Anatoa muhtasari wa namna alivyoshiriki katika mambo mengi ambayo
yalichangia katika kubadili sekta ya mawasiliano Tanzania.
Anaongea kwa hamasa kuhusu umuhimu wa usimamizi makini wa mifumo ya mazingira ambapo
anaeleza namna bora ya kushughulikia utupaji wa taka za kielektroniki kwa kujifunza kutoka uzoefu wa
nchi nyingine ambazo zimefanikiwa katika eneo hili.
Masimulizi haya ya Mhandisi Kilaba yatawapa motisha wasomaji – vijana na wazee – kuhusu namna ya
kujitahidi kufikia ndoto changamani za maisha. Ni zawadi kwa wasomaji ambao watapata fursa ya
kupata uzoefu wa mtaalamu wa TEHAMA aliyebobea ambaye sasa ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Kitabu hiki ni cha kipekee – kwa mtindo, maudhui na kinavyoonekana. Kimechanganya masimulizi mithili
ya hadithi na uchambuzi wa kina wa kitaalamu kuhusu masuala mbalimbali. Maudhui yake
yametafsiriwa kwa Kiingereza na kuchapishwa kama kitabu pekee.
Hii inakipa sifa ya kamusi ya haraka ya istilahi za kitaalamu na pia kama rejea muhimu.

Seller | KILABABOOKSTORE |
---|---|
Total Pages | 228 |
Publisher | Inland Press and Publishers, Mwanza, Tanzania. |