Urafiki na Uchumba
Safari ya ndoa huanza na uhusiano. Uhusiano
unaanza kwa kufahamiana. Kufahamiana
kunaanza na urafiki. Mtu anaweza kukupenda,
lakini si muhimu awe rafiki, kwani marafiki
huchaguliwa. Watu wengi wanaingia katika
uhusiano wakiwa na matazamio mengi pasipo
maandalizi ya kutosha.
Safari ya ndoa huanza na uhusiano. Uhusiano unaanza kwa kufahamiana. Kufahamiana kunaanza na urafiki. Mtu anaweza kukupenda,
lakini si muhimu awe rafiki, kwani marafiki huchaguliwa. Watu wengi wanaingia katika uhusiano wakiwa na matazamio mengi pasipo
maandalizi ya kutosha. Kuna matatizo mengi yanayotokea katika ndoa nyingi siku hizi. Uzoefu unaonesha kuwa, matatizo mengi yanayopelekea
kuvunjika kwa ndoa nyingi yanatokana na sababu kuu tatu zifuatazo;
• Kukosekana kwa maamuzi makini wakati wa kutaka kuoa au kuolewa.
• Malezi na makuzi mabaya wakati wa utoto.
• Kukosekana kwa ufahamu na maarifa ya kutosha kuhusu taasisi ya ndoa.
Maisha ni hatua. Maisha yenye mafanikio yanahitaji utaratibu, subira na uvumilivu. Vijana wengi siku hizi huanza uhusiano wa kimapenzi
mapema kabla ya ndoa. Hivyo, inapofika hatua ya kufunga ndoa huwa hakuna jipya.Wengi wao
wanakuwa wamezoeana, bahati mbaya sana hata kutubu kwa mwenyezi Mungu wanasahau. Hali ilivyo sasa, vijana wengi wameoa au kuolewa
na watu wasio halisi na sahihi. Wako waliohusiana na watu ambao wamekuwa vikwazo katika maisha yao. Wengi wamehusiana na watu ambao
wamefisha ndoto zao, malengo na maono yao; wameua imani katika Mungu na kuondoa furaha yao.
Kukurupuka, matazamio yasiyo halisia, ulevi wa mapenzi na kukosa umakini vimewagharimu vijana wengi. Vijana wengi hawafahamu tofauti
iliyopo kati ya kipindi cha urafiki na kipindi cha uchumba. Tunashuhudia siku hizi vijana wengi wakiwa wachumba na kuamua kuoana
hata bila kupitia hatua ya urafiki. Ni muhimu ifahamikie kuwa, kipindi cha urafiki ni kipindi cha kumfahamu mtu vizuri zaidi kuliko kipindi cha
uchumba, kwani wakati wa uchumba watu wengi huficha uhalisia wao. Majira ya urafiki na uchumba ni tofauti. Kijitabu hichi cha urafiki na uchumba kitawasaidia vijana kujitambua na kutofautisha majira ya urafiki na uchumba ili kufanya maamuzi sahihi kwa wakati
sahihi na kwa mtu sahihi.
Seller | MLYUKA BOOK STORE |
---|---|
Author | Rev.Dr. Enock E Mlyuka |
Good Read | Yes |
Total Pages | 33 |
Publisher | Rev.Dr.Enock E Mlyuka |