Ushindi Katika Vita Ya Kiroho na Mwl. Eng. Peniel Sarakikya
Ukitaka kuwa shujaa wa Imani lazima utambue nafasi ya
Roho Mtakatifu na umruhusu akusaidie mapiganoni.
Hapo ndipo utashinda, naam, na zaidi ya kushinda.
Yesu Kristo aliyefufuka hufunuliwa katika utukufu, nguvu,
ushindi na utakatifu. Mungu amelikusudia kanisa kuwa
lenye utukufu, nguvu, ushindi na utakatifu katika
ulimwengu wa sasa na sio kanisa nyonge.
Matumizi sahihi ya damu ya Yesu ndilo Pigo kuu na la
mwisho katika pambano lolote la kiroho. Kuna nguvu kuu
katika damu ya Yesu. Kuna Ukombozi katika damu ya
Yesu (Efe 1:7).
Kuna kibali cha kumkaribia Mungu katika damu ya Yesu
(Ebr 10:19, Efe 2:13). Kuna uponyaji katika damu ya Yesu
(Isa 53:5).
Kuna ulinzi katika damu ya Yesu (Kut 12:13). Kuna
mamlaka ya kumshinda shetani ndani ya damu ya Yesu
(Ufu 12:11).
Pigo la mwisho katika vita yoyote ya kiroho ni damu ya
Yesu. Unapoitumia damu ya Yesu kwa usahihi
HUTASHINDWA VITANI KAMWE.
Kwa kuwa Mungu hapendi kuona unashindwa vitani,
ameweka kitabu hiki mikononi mwako kikusaidie kuishi
maisha ya ushindi.
Bwana Yesu asifiwe milele.
Mwaka 2018 nilisikia sauti ya Mungu ikinielekeza
kuandika somo hili. Nilianza kuandika kama mfululizo
makala gazetini.
Baadaye nikazikusanya zile makala na kuandaa toleo la
kwanza la kitabu hiki mwaka 2020 Julai. Na sasa, toleo hili
la pili la mwaka 2024 ni matokeo ya kuboresha na
kuondoa makosa ya uchapaji yaliyokuwepo kwenye
toleo la kwanza.
Maisha ya mwanadamu ni uwanda mapambano endelevu
yasiyoisha. Inawezekana hata wewe ni shahidi, kwamba
kuna wakati ulishindwa katika jambo ambalo
ulijihakikishia ushindi. Jambo ambalo ulishindwa na
hukuwa na maelezo ya kutosha kwanini ulishindwa.
Kuna uwezekano kwamba ulishindwa kwa sababu ya vita
inayokukabili katika ulimwengu wa roho. Isingekuwa ni
hiyo vita, ungeshafanikiwa katika mambo mengi.
Kushindwa kuelewa yanayoendelea katika ulimwengu
wa roho ni sababu ya wengi kushindwa. Ushindi katika
vita vya kiroho unategemea mambo makuu matatu.
a. Kwanza, ni uelewa wako kuhusu pande mbili
zinazopigania kuyadhibiti maisha yako.
viii
b. Pili ni kujua silaha za ushindi na matumizi yake
sahihi.
c. Na tatu, ni kujua kanuni mbali mbali za ushindi
katika vita vya kiroho.
Haya ndiyo mambo ambayo utajifunza kwa undani sana
katika kitabu hiki, kwa kuwa hiki ni kitabu cha washindi.
Ukitaka kuishi maisha ya ushindi duniani, jifunze jinsi
shetani anavyomshambulia mwanadamu, kisha jifunze
namna Mungu anavyotusaidia kumshinda.
Chuki na hasira ya Shetani dhidi ya mwanadamu
inalenga mambo makuu mawili.
Kwanza kabisa, shetani anamshambulia mwanadamu ili
kumzuia asiweze kumiliki na kutawala hapa duniani. Pili
kumzuia mwanadamu asiweze kuurithi uzima wa milele
alioandaliwa na Mungu.
Usipokuwa tayari kulinda ulichonacho, kuna siku
utalazimika kupigana ili kukomboa ulichonyang'anywa
na shetani. Kinga ni bora kuliko tiba.
Uwepo wa mateka, majeruhi na wasaliti katika vita vya
kiroho ni kiashiria kingine cha namna ulimwengu wa
roho unavyojaribu kuyadhibiti maisha ya mwanadamu.
Vita vya kiroho ni vita endelevu.
Hii ni sababu mojawapo ya kwanini Biblia imeonyesha
silaha nyingi za kujilinda, na silaha moja ya kushambulia.
Adui shetani hupambana na mwanadamu akitumia falme,
mamlaka, wakuu wa giza na majeshi ya pepo wabaya
katika ulimwengu wa roho.
Shetani, malaika walioasi na pepo wachafu wana nguvu
fulani ila hawana mamlaka ya kutawala dunia kwa kuwa
hawana mwili wa damu na nyama. Ili kupata uhalali
hutumia wanadamu na wanyama kufanya kazi zake.
Mlango mkuu wanaotumia ni ujinga wa mwanadamu na
uasi wa mwanadamu mbele za Mungu. Ushindi wa
shetani unategemea ujinga wa mwanadamu wa
kutokujua Neno la Mungu.
Yapo mapambano matatu ambayo kama askari lazima
ujiandae kukabiliana nayo. Vita kati ya roho yako na
mwili wako. Vita kati yako na ulimwengu, kisha vita kati
yako na shetani.
Shetani hatakuacha upigane na mwili hadi umalize kabla
hujaanza kupigana na ulimwengu na maadui wengine
rohoni. Wakati roho yako inapigana na mwili wako
ulimwengu utakushambulia.
Wakati unapigana na mwili na ulimwengu kwa pamoja,
shetani naye atakushambulia. Vita zote hizi tatu hutokea
kwa wakati mmoja ndio maana huwezi na usitarajie
kushinda bila msaada wa Roho Mtakatifu.
Ukitaka kuwa shujaa wa Imani lazima utambue nafasi ya
Roho Mtakatifu na umruhusu akusaidie mapiganoni.
Hapo ndipo utashinda, naam, na zaidi ya kushinda.
Yesu Kristo aliyefufuka hufunuliwa katika utukufu, nguvu,
ushindi na utakatifu. Mungu amelikusudia kanisa kuwa
lenye utukufu, nguvu, ushindi na utakatifu katika
ulimwengu wa sasa na sio kanisa nyonge.
Matumizi sahihi ya damu ya Yesu ndilo Pigo kuu na la
mwisho katika pambano lolote la kiroho. Kuna nguvu kuu
katika damu ya Yesu. Kuna Ukombozi katika damu ya
Yesu (Efe 1:7).
Kuna kibali cha kumkaribia Mungu katika damu ya Yesu
(Ebr 10:19, Efe 2:13). Kuna uponyaji katika damu ya Yesu
(Isa 53:5).
Kuna ulinzi katika damu ya Yesu (Kut 12:13). Kuna
mamlaka ya kumshinda shetani ndani ya damu ya Yesu
(Ufu 12:11).
Pigo la mwisho katika vita yoyote ya kiroho ni damu ya
Yesu. Unapoitumia damu ya Yesu kwa usahihi
HUTASHINDWA VITANI KAMWE.
Kwa kuwa Mungu hapendi kuona unashindwa vitani,
ameweka kitabu hiki mikononi mwako kikusaidie kuishi
maisha ya ushindi.
Ni maombi yangu kwa Mungu kwamba kupitia kitabu hiki
utapata msaada wa kukutoa hapo ulipokwama. Ni shauku
yangu kuona kitabu hiki kinakuweka karibu zaidi na Yesu
Kristo na kumruhusu yeye awe Bwana na mwokozi wa
maisha yako.
Kula na ukue kiroho.
Asifiwe Yesu kabisa.
Mwl. Eng. Peniel S. Sarakikya
Aprili, 2024
Seller | SARAKIKYABOOKSTORE |
---|---|
Author | Mwl. Eng. Peniel Sarakikya |
Total Pages | 184 |
Publisher | Kiwonyi Printers |
-
Knowing Jesus Christ by Mwl. Eng. Peniel SarakikyaTZS 10,000.00