Wokovu na Dini Na Dr A Mmanyi

TZS 10,000.00
In stock
SKU
SplWokovu by Dr A Mmanyi

Wokovu na Dini

Katiba dunia hii yenye msitu mkubwa wa dini na madhehebu, swali linalowatatiza wengi ni “je ni dini ipi sahihi ya kumpeleka mtu kwa Mungu?” Hata hivyo, ni wachache wanaouliza swali la msingi: “Je, dini inaweza kumpeleka mtu kwa Mungu?” Hakuna haja ya kupoteza muda kuchagua dini inayofaa kumpeleka mtu mbinguni kabla ya kujua kama dini yenyewe ina uwezo wa kufanya hivyo. Kitabu hiki cha Dr. Mmanyi kinadadavua kwa kina na kwa msingi wa maandiko kwamba dini pekee haina uwezo wa kumfikisha mtu mbinguni, bali wokovu kupitia Bwana na Mwokozi, Yesu Kristo.

Licha ya ukweli huo, Dr. Mmanyi, ambaye pia ni muumini mwaminifu wa dini yake ya Kikristo, habezi uwepo wa dini bali anajadili kwa kina nafasi yake na umuhimu wake katika maisha ya mtu. Kitabu hiki kinatoa mbinu maalum za kuimarisha umoja na mshikamano, unaojengwa kwenye msingi wa mambo yanayofanana badala uhasama na miganyiko inayotokana na tofauti zetu

Aron Mwasile
Mkurugenzi, INcontext Tanzania

Links

MAMBO MUHIMU YALIYOPO KWENYE KITABU CHA WOKOVU NA DINI

>Maana ya dini, udini na udhehebu

>Maana ya wokovu na unavyopatikana

>Wokovu na maendeleo

>Ubatizo na tafsiri ya ubatizo wa mtoto mdogo 

>Mafundisho maalumu kuhusu sadaka ya mavuno, pasaka na sadaka ya shukrani baada ya kufiwa

>Kurasa maalumu zenye riwaya 13 za mahubiri

More Information
Seller DRMMANYIBOOKSTORE
Author Dr Allyson M Mmanyi
Total Pages 154
Publisher Aims (2020) Press
Write Your Own Review
You're reviewing:Wokovu na Dini Na Dr A Mmanyi
Your Rating
Copyright © 2023 - 2024 Mahali Sokoni Trading Company Limited. All rights reserved.