Zoezi na Mazoezi ya Akili - Theofano Mbuye
Humuwezesha kila mmoja wetu sio tu kufundishwa, bali na kujifunza kuendelea kuishi vizuri katika maisha yetu kila mtu, mimi na wewe wenyewe binafsi kwanza na kati ya mtu mwingine yeyote na watu wengine wowote mahali popote. Kupitia miili yetu ya kibinadamu kila mmoja wetu kutoka mioyoni mwetu wakati tunaishi duniani. Mfano, katika maisha ya familia, ndoa, uchumba, urafiki, ujirani, ndugu na tunaojumuika nao kazini au kwenye shughuli zetu au matukio ya kijamii, kitaifa na kimataifa.
Ni mazoezi tiba kwa mtu yeyote husika unayoendelea kuyatumia vizuri, kuboresha na kuimarisha akili na Roho. Ili mtu husika uendelee kuwa mwenye nguvu thabiti ya akili na Roho na mwenye hali njema ya afya bora ya akili na Roho. Katika hali endelevu ya kutumia ujuzi wetu na mbinu zetu, kuendelea kuishi vizuri na mtu yeyote. Wewe mwenyewe binafsi na kati yetu watu wote ndugu na tusiondugu, kwenye mambo na matukio mbalimbali ya maisha wakati tunaishi duniani hata wakati hatuishi duniani.
Katika hali ya kuepuka kuendelea kutumia ujuzi wa dhidi yetu na mbinu za dhidi yetu za mtego wa kuendelea kuishi vibaya na mtu yeyote.
Wewe mwenyewe binafsi na kati yetu watu wote ndugu na tusiondugu, kwenye mambo na matukio mbalimbali ya maisha wakati tunaishi duniani hata wakati hatuishi duniani.
Seller | theofanombuyebookstore |
---|---|
Author | Theofano Mbuye |
Good Read | No |
Total Pages | 113 |
Publisher | SpringPlay |